Searching...
Jumatano, 29 Mei 2013

BUSTANI ZA BIASHARA ZA MAUA JIJINI DAR ES SALAAM CHANZO CHA UCHAFUZI NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

 Maua mazuri,yanavutia,ukiyaona unatamani usimame uyanunue upeleke nyumbani kwako ila chanzo chake kimeelezwa kuwa ni uharibifu wa mazingira.
 Hili ni eneo pembezoni mwa barabara ya cocacola mwenge jijini dar es salaam ambalo pande zote mbili za barabara zinatumiwa na wajasiriamali wa kilimo cha maua.
 hilo ni bwawa au dimbwi lililochimbwa pembezoni mwa barabara hiyo ya cocacola jijini dar es salaam ambalo linadaiwa kuwa uchafuzi na uharibifu wa mazingira.
Hiyo ni  moja ya jamii ya maua yanayolimwa pembezoni mwa barabara hiyo.
 Yapo maua ya aina mbali mbali ambayo kwa hakika kama wangekuwa na vyanzo vizuri vya umwagiliaji yangependezesha sana mandhari ya barabara na jiji kwa ujumla.
 Hapa ndipo mambo yanapoharibika,...hapa wajasiriamali wameamua kufunga mtaro ili kuzuia maji yasiende ili wapate maji ya kumwagilia,kama serikali inaona hii biashara ni sawa basi iwawezeshe wajasiriamali hawa visima vya maji ili wasiharibu mazingira na miundombinu ya maji machafu.
 Mtaro ukiwa umezibwa na mawe na matakataka kama unavyoona picha ya juu na chini
 Ila bustani zimependeza
 Hiyo ndiyo taswira sahihi ya mtaro huo uliozibwa.

Na hivi ndivyo hali ya uchafu ilivyo katika mitaro inayotumiwa na wajasiriamali wa kilimo cha maua jijini Dar es salaam barabara ya cocacola mwenge.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!