Searching...
Jumamosi, 20 Aprili 2013

WAZAZI WAENDELEA KUCHANGISHWA CHAKULA CHA WANAFUNZI NJOMBE

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjrDd8ItSU0zMmROryi-IBpL7JX-xnSzHapBVtZ5r-S2Aa5KSjkI0GnNEGrLXJvMAKDatVqbCRfJpfoG09yE2n8L2UiKqtZWgdYVHQwwVRQqB47NqPH0cbYC5S9fMnCNMu4Wa0Ajw8n80R1/s1600/P1090687.JPG
 hawa ni baadhi ya wazazi waliolalamikia kutumia migambo kuzunguka na wanafunzi kwenda kuonesha nyumba zao kwa ajili ya michango ya chakula shuleni.
 Hawa ni baadhi ya Wazazi waliolalamikia watoto wao kurudishwa na migambo kuonesha nyumba zao ili kuchangia chakula April 16 mwaka huu.
 Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mabati Njombe Bi.Elizabeth Mhonjwa akieleza kilichopelekea kutumia njia mbadala ya kuwatafuta wazazi baada ya serikali ya mtaa kushindwa kufanikisha zoezi hilo.
 Hapa ni eneo la Shule la Nyuma ambako mwalimu mkuu wa shule hiyo amepanda miti aina ya Parachichi takribani 20 kwa ajili ya Mradi wa Shule.
 Baada ya nguvu ya Mgambo kutumika kuwatafuta wazazi ambao hawajachangia chakula shuleni hatimaye chakula chapatikana na kinapikwa ili wanafunzi waendelee kula.
Mmoja wa Mgambo aliyetumika kuzunguka na watoto kwenda kuonesha nyumba zao ili kudai michango ya chakula kwa wazazi baada ya serikali ya mtaa kushindwa kuwapata wazazi.
Huyu ni Afisa mtendaji wa Mtaa wa SIDO na Buguruni Mjini Njombe Bi.Rehema Ngailo akieleza uamuzi wa kamati ya shule kufikia hatua ya kutumia mgambo kuwasaka wazazi nyumbani kwao.Picha zote na Gabriel Kilamlya.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!