Searching...
Ijumaa, 19 Aprili 2013

JAMII YAFAIDIKA NA MAFAO YA NSSF

Ofisa wa Matibabu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Yasinta Shibola akitoa ufafanuzi kwa watu mbambali waliotembelea banda la NSSF wakati wa maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam leo ambapo NSSF ni moja ya taasisi zinazoshiriki katika maonesho hayo. 
Baadhi ya watu mbalimbali wakipata maelezo ya huduma zinazotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na hasa huduma ya mafao ya matibabu iliwafutia watu wengi, wakati wa maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Uhusiano Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Maife Kapinga akifafanua jambo kuhusu huduma ya mafao ya matibabu wakati wa maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya watu waliojitokeza katika banda la NSSF wakipata maelezo ya huduma mbalimbali za NSSF.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!