Mstahiki Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akilakiwa na uongozi wa Starkey
alipowasili katika shule ya Buguruni Viziwi kuzindua kambi ya Starkey
itakayokuwa inatoa huduma ya uchunguzi, vifaa na matibabu bure kwa
wananchi wenye matatizo ya kusikia.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo na mmoja wa wauguzi katika kambi hiyo mara baada ya kuwasili.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa
akifanyiwa uchunguzi wa tatizo la kutosikia wakati kuzindua kambi ya
Starkey itakayosaidia kutoa huduma na matibabu bure kwa wananchi wenye
matatizo ya kusikia iliyopo kwenye shule ya watoto wenye ulemavu wa
kusikia (Buguruni viziwi) jijini Dar.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh.Jerry Silaa
jana tarehe 16 April 2013 amezindua kambi ya Starkey ya kusaidia wananchi
wenye matatizo ya kusikia iliyofanyika katika shule ya watoto wenye
ulemavu wa kusikia (Buguruni viziwi), ambapo wenye magonjwa watatibiwa
na wenye kuhitaji vifaa vya kuongezea usikivu watatengenezewa kulingana
na size zao na watapewa bureee.
Mstahiki Meya amepima na kwa kuwa ameonekana kutokuwa na tatizo
amepata fursa ya kutengenezewa "custom made earphones" wote wenye
matatizo mnakaribishwa. Huduma hii ni bureee...
Picha juu na chini ni Mstahiki
Meya Jerry Silaa akivishwa "Custom made earphones" na mmoja wa madaktari
bingwa katika kambi hiyo mara baada ya kuzindua huduma hiyo atakayokuwa
ikitolewa bure kwa wananchi wenye matatizo ya kusikia.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akimsalimia mmoja wa watoto waliofika kambini hapo kupatiwa huduma baada ya kuizindua.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo ya namna huduma hiyo itakavyokuwa ikitolewa kwa wagonjwa watakaofika kambini hapo.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa kambi hiyo mara baada ya kuzindua.
0 comments:
Chapisha Maoni