Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule kwa pamoja na Bibi Petra
Hammelmann, Mwakilishi wa Heshima Mteule wa Tanzania mjini Hamburg
nchiniUjerumani wakisaini Mkataba wa kumwezesha Bibi Hammelmann kuwa
Mwakilishi wa Heshima rasmi wa Tanzania katika mji huo. Mkataba huo
ulisainiwa Wizarani tarehe 16 Aprili, 2013.
Bw. Haule na Bibi Hammelmann wakibadilishana mkataba huo mara baada ya kusaini.
Bw. Haule kwa pamoja na Bibi Hammelmann wakionesha mkataba huo.
Bw. Haule akizungumza na Bibi
Hammelmann mara baada ya kusaini mkataba utakaomwezesha Bibi Hammelmann
kuwa Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania mjini Hamburg. Pamoja na mambo
mengine Bw. Haule alimhimiza Mwakilishi huyo kutangaza vivutio vya
utalii vya Tanzania mjini Hamburg ili kukuza sekta ya utalii hapa
nchini.
Bw. Haule akiendelea na mazungumzo na Bibi Hammelmann huku Bw. Mwandembwa na Bw. Ali wakisikiliza.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Andy
Mwandembwa (kushoto) pamoja na Bw. Ali Ubwa, Afisa Mambo ya Nje kutoka
Kitengo cha Sheria wakishuhudia uwekaji saini huo.Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiririkiano wa Kimataifa
0 comments:
Chapisha Maoni