Mshambualiaji wa Liverpool Luis Suarez 26, hatoichezea tena klabu yake ya sasa Liverpool baada ya kufungiwa michezo kumi na inasemekana atajaribu kulazimishakuondoka klabuni hapo katika kipindi cha majira ya joto.
Full story: Daily Star
Kocha wa klabu ya soka ya Hispania ya Real Madrid mreno Jose Mourinho amekubali kurejea katika klabu yake ya zamani ya England ya Chelsea na inasemekana atatua stamford Bridge akiwa pamoja na mshambuliaji wa Atletico Madrid Radamel Falcao, 27.
Full story: Bild (in German)
Baba mzazi wa mchezaji kinda wa brazil Neymar 21,pamoja na wakala wake wamesema mwakani Neymar atakwenda kukipiga na klabu ya Hispania ya Barcelona baada ya ofa za Chelsea na real madrid.
Full story: Daily Mail
Mlinzi kisiki na kapteni wa klabu ya Chelsea John Terry, 32,amesema ana furaha kuhusu maisha yake ya baadae ndani ya klabu hiyo tajiri yenye makao yake makuu Stamford Bridge, achilia mbali kutakiwa na vilabu mbalimbali ulaya.
Full story: Daily Express

Mkurugenzi mkuu wa Manchester United David Gill amewaonya majira zao Manchester City kwamba kocha wake Sir Alex Ferguson atakiimarisha kikosi chake mara dufu baada ya dirisha la usajili litakapo funguliwa. Full story: Manchester Evening News
Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Manchester city Scott Sinclair 24,amesema yupo tayari kuondoka kwa mkopo klabuni hapo msimu ujao endapo kocha wa klabu hiyo Roberto Manchini hatofukuzwa.
Full story: Daily Mirror
Klabu ya arsenal wameonyesha nia yao ya kutaka kumsajili mchezaji wa muajentina mlinzi Federico Fazio 26.
Full story: Daily Mail
Kocha wa Everton David Moyes yupo katika vita kali na manchester City kumgombea mlinzi wa Leeds Sam Byram, 19.
Full story: the Sun
Mchezaji bora wa dunia Lionel Messi 25, anayekipiga katika klabu ya Barcelona amesema watajitahidi kwa nguvu na uwezo wao wote kufanya lile lisilowezekana kuwafunga Bayern Munich wiki ijayo watakapotua nou Camp ili waweze kutinga fainali.
Full story: the Independent
Mshambuliaji wa Chelsea Fernando Torres 29, amesisitiza kwamba ataendelea kukipiga klabuni hapo msimu ujao na kuahidi kuwakaribisha wachezaji wengine nyota watakaosajiliwa klabuni hapo.
Full story: The Times (subscription only)
0 comments:
Chapisha Maoni