Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone(katikati) akifungua mkutano wa maelewano katia ya kampuni ya JEO na Wind East Africa, zinazotarajiwa kuzalisha umeme wa upepo katika manispaa ya Singida, viongozi wa NDC,Tanesco makao makuu na viongozi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Singida.Naibu waziri wa nishati na madini Mh. George Simbachewene (wa kwanza kushoto) ndiye aliyeitisha mkutano huo.Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Singida, Mwl.Queen Mlozi.
Mkurugenzi wa kampuni ya Wind East Africa, Rashidi Shamte akitoa nasaha zake kwenye mkutano huo wa maelewano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida.
Afisa mwanadamizi wa shirika la Tanesco ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akitoa nasaha zake kwenye mkutano wa maelewano wa kampuni ya JEO na Wind East Africa.
Baadhi ya maafisa waandamizi wa kampuni ya Wind East Africa wakifuatilia kwa makini mkutano wa maelewano kati yao na wale wa JEO.
Baadhi wa viongozi wa shirika la Tanesco wakifuatilia kwa makini mazungumzo yaliyohusu maelewano kati ya kampuni ya Wind East Africa na JEO yanayotarajiwa kuanza kuzalisha umeme wa upepo katika manispaa ya Singida.
Naibu waziri wa nishati na madini Mh. George Simbachawene akihutubia wakazi wa kijiji cha Januka manispaa ya Singida.Mh. Simbachewene alifanya ziara katika kijiji hicho kukagua maendeleo ya mradi wa kufua umeme wa upepo.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Januka manispaa ya Singida wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na naibu waziri wa nishati na madini  Mh. George Simbachawene (hayupo kwenye picha).Mkutano huo uliofanyika kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumzia mradi wa kufua umeme wa upepo kijijini hapo.
(Picha zote na Nathaniel Limu).