Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema mitambo ya Analojia mkoani Mbeya itazimwa rasmi leo saa 6:00 usiku.
Akizungumza na waandishi habari Meneja
Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi,
amesema Mkoa wa Mbeya umekuwa wa mwisho katika hatua za kuzima mitambo
hiyo, katika awamu ya kwanza.
Mungi alisema uzimaji wa mitambo ya analojia na
kuhamia katika mitambo ya Digitali katika awamu ya kwanza, ulihusisha
Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Tanga, Mwanza, Moshi na Arusha.
Amesema wakazi wa Mbeya walikwishafahamishwa
kuhusu kuzimwa kwa mitambo hiyo kwa kufanya maandalizi yaliayohitajika
ili kuepuka usumbufu ambao ungejitokeza.
Aliwataka Watanzania kuacha
kunung’unika wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali na hasa yanayohusu
matatizo ya ving’amuzi na badala yake, wachukue hatua za kutafuta ufumbuzi
Alisema
baadhi ya Watanzania wamekuwa wakitumia muda mrefu kunung’unika na
kushindwa kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
0 comments:
Chapisha Maoni