Amina Mkombe na Mwanajuma Mkombe wakisoma utenzi kusherehesha kwenye usinduzi wa wiki ya usalama bara barani zilizofanyika katika ukumbi wa salama katika hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
 Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa akitoa takwimu za ajali na vifo kwa mwaka 2012 na 2012 kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama bara barani zilizofanyika katika ukumbi wa salama  bwawani hoteli.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr. Saleh Mohammed Jidawi akitoa takwimu za vifo na majeruhi waliopokelewa katika vituo mbali mbali vya afya hapa Zanzibar kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama bara barani hapo bwawani hoteli.
Mwakilishi wa Wizara ya elimi Zanzibar Bwana  Ahmed Abdull majid akielezea madhara wanayoyapata wanafunzi waendapo maskulini wakati wanapotumia bara bara kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama bara barani hapo bwawani Hoteli.
Katibu Mkuu Wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano Dr. Juma  Malik akielezea juhudi zinazochukuliwa na Wizara yake katika kuendeleza miundo mbinu ya bara bara ili kupunguza ajali.
Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasiliano Zanzibar Mh. Rashid Seif akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya usalama bara barani hapo Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizindua wiki ya usalama bara barani hapo katika ukumbi wa salama hoteli ya bwawani Mjini Zanzibar.
Baadhi ya washiriki walioshuhudia uzinduzi wa wiki ya usalama bara barani zilizofanyika katika ukumbi wa salama hoteli ya bwawani Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Kudumu ya usalama bara barani Mh. Abdulla Mwinyi ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi akitoa shukrani mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa wiki ya usalama wa bara barani hapo bwawani Hoteli Mjini Zanzibar.Picha Hassan Issa wa  - OMPR – ZNZ.