Korea Kaskazini imehamisha makombora mengine kwenye mwambao wake wa
Mashariki tayari kwa mashambulizi dhidi ya Marekani, huku nchi hiyo
inayotishiwa kushambuliwa ikisema inachukua tahadhari kubwa kutokana na
vitisho hivyo.
Kulingana na chombo cha habari cha Yonhap cha Korea Kaskazini kikimnukuu
afisa mmoja wa serikali nchini humo, kimesema makombora mawili tayari
yameshasafirishwa kwa treni mapema wiki hii na kuwekwa katika magari
tayari kwa kushambulia.Kwa upande wake Wizara ya ulinzi ambayo ilithibitisha kupelekwa kwa kombora la kwanza ilikataa kutoa maoni yake juu ya habari za hivi karibuni kwamba makombora mengine yamesafirishwa Mashariki mwa pwani ya nchi hiyo.
Hata hivyo afisa mmoja wa jeshi amekiambia chombo hicho cha Yonhap kwamba, makombora yaliyosafirishwa yametegeshwa Mashariki na Magharibi mwa pwani ya Korea Kaskazini.
Vitisho hivyo vya Korea kaskazini ni mojawapo ya misururu ya vitisho vya wiki kadhaa sasa, kufuatia vikwazo vya Umoja Wa Mataifa dhidi yake na mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea kusini.
Habari hii kwa hisani ya DW Swahili
0 comments:
Chapisha Maoni