RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.Jakaya Kikwete
amemtumia salamu za rambirambi Makamu wa Rais Dr.Mohamed Gharib Bilal
kuomboleza kifo cha mdogo wake, Haji Gharib Bilal kilichotokea Aprili
16, 2013.
Katika salamu zake za rambirambi, Rais Kikwete amemwambia Makamu wa
Rais: Nimepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa ya kifo cha mdogo
wako, Haji Gharib Bilal, ambaye nimejulishwa kuwa amepoteza maisha
nchini Oman akiwa njiani kupelekwa India kwa matibabu.”
“Ndugu Haji Gharib Bilal alikuwa mtu aliyeheshimiwa sana na wenzake
na jamii katika duru za shughuli za biashara ambayo alijihusisha nayo
maisha yake yote. Nakutumia wewe Mheshimiwa Makamu wa Rais salamu za
rambirambi za dhati ya moyo wangu kufuatia msiba huu mkubwa kwako wewe
binafsi na kwa familia nzima. Naungana nawe katika maombolezo.”
Ameongeza Rais: “Aidha kupitia kwako nawatumia salamu zangu za rambirambi wanafamilia ya Marehemu Haji Gharib Bilal akiwamo mjane na watoto wake watatu. Napenda kukuhakikishia kuwa niko nawe Mheshimiwa Makamu wa Rais na familia nzima katika wakati huu mgumu wa kuomboleza kifo cha ndugu yetu. Namwomba Mwenyezi Mungu awape nguvu, uvumilivu na subira za kuweza kuhimili machungu ya kipindi hiki.”

Amesisitiza Mheshimiwa Rais, “aidha, naungana nanyi katika kumwomba
Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya marehemu Haji
Gharib Bilal. Amina.”
0 comments:
Chapisha Maoni