Searching...
Alhamisi, 25 Aprili 2013

JENGENI TABIA YA KUPIMA UGONJWA WA KISUKARI-DR.MWINYI



 1
 WAZIRI WA AFYA MH.DR.HUSSEIN MWINYI

 IMEELEZWA kwamba inakadriwa kuwa asilimia saba ya idadi ya watu wazima wanaugua ugonjwa wa kisukari, lakini chini ya 1/3 ndio wanaofahamu wana tatizo hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (Pichani) wakati akizindua kliniki ya vikoba ya wagonjwa wa kisukari uliofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dares Salaam.
Dk. Mwinyi alisema watu wanaokabiliwa na tatizo hilo, wanafika hospitalini wakiwa wameathirika figo, macho, shinikizo la damu au kukatwa miguu.
“ Ninaishauri jamii kutumia huduma hiyo ili kuweza kuchunguza afya zao na kujinga kwa kufuata kanuni za afya kama vile kula vyakula visivyo na mafuta mengi, sukari nyingi, chumvi kiasi, kula mboga za majani kwa wingi na matunda,” alisisitiza. Dk. Mwinyi.
Aliongeza pia jamii inatakiwa kufanya mazoezi ya kutosha, kupunguza uzito kwa kiwango kinachotakiwa, kutovuta sigara na kupunguza kunywa pombe au kuacha kabisa.
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!