Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,wama, Mama
Salma Kikwete akipokewa rasmi na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Jhpiego
nchini Tanzania, Bi Maryjane Lacoste kwenye hoteli ya Doubletree huko
Masaki kulikofanyika sherehe ya kutimiza miaka 40 ya shirika hilo tarehe
23.4.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Dr. Maryrose
Giattas, Cervical Cancer Prevention Program Adviser wa Shirika la
Jhpiego kwenye maonyesho ya huduma mbalimbali zitolewazo na shirika
hilo. Maonesho hayo yalifanyika katika hoteli ya Doubletree ikiwa ni
sehemu ya kusherehekea miaka 40 ya shirika hilo.
Mama
Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Dr. Hokororo wa shirika la
JHPiego juu ya kuhifadhi vifaa vinavyotumika katika suala zima la afya
ya mama na mtoto.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na baadhi ya viongozi waliohudhuria
sherehe ya kutimiza miaka 40 ya shirika la Jhpiego huko Doubletree hotel
Masaki. Kulia kwa Mama Salma ni Dr. Leslie Mancuso, Rais na Mtendaji
Mkuu wa Jhpiego akifuatiwa na Bi Sharon Cromer, Mkurugenzi wa Shirika la
USAID nchini Tanzania. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Seif Rashid akifuatiwa na Dr Allan Damiba, Jhpiego Senior Vice
President na wa mwisho ni Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Sophia
Mjema, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
0 comments:
Chapisha Maoni