Ofisa
Maendeleo wa Kusini mwa Afrika wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA), Ashford Mamelodi (kushoto) akisistiza jambo jana
alipotembelea wizara ya Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo Bw.Seth Kamuhanda
wa kwanza kulia akimsikiliza mwakilishi wa Fifa wa kwanza kushoto
aliyekuja nchini kutatua mgogoro uliokuwepo kwenye uchaguzi wa rais wa
shirikisho la mpira nchini katikati ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) Bw.Leodgar Tenga katika ukumbi wa Wizara ya Habari
jana jijini Dar es salaam.
Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari,
,Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Loenard Thadeo kushoto kwake ni
Mkurugenzi Wa Habari Bw.Assah Mwambene,Mkurugenzi wa Msaidizi wa Michezo
Bi.Juliana Yasoda na Afisa Habari Mkuu wa Wizara Bw.Godlease Malisa
wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bw.Seth Kamuhanda hayupo kwenye
picha .
Wawakilishi
wa fifa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bw.Seth Kamuhanda aliyekaa Katikati
na baadhi ya viongozi wa wizara na Shirikisho la mpira wa Miguu (TFF)
wakiongozwa na Rais Leodgar Tenga aliyeketi wa Kwanza Kushoto.
0 comments:
Chapisha Maoni