Searching...
Jumanne, 16 Aprili 2013

ANGALIA PICHA 12 ZIKIONYESHA JINSI WANAFUNZI 25 WALIVYONUSURIKA KUFA LEO IRINGA KATIKA AJALI MBAYA YA GARI.



WANAFUNZI zaidi ya 20 wa shule ya kimataifa ya St Charles iliyopo Don Bosco katika Manispaa ya Iringa wamenusurika kifo baada ya gari waliyokuwa wamepanga aina ya Daladala lenye namba T415 AEG kushindwa kupanda mlima na kupinduka.
Huku mbinu za wezi wa watoto zikionyesha kugonga mwamba baada ya mwanamke mmoja kushtukiwa akitaka kukimbia na mtoto asiye wake kwa madai anamkimbiza Hospitali.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 2 mchana wa leo katika eneo la Msikiti wa Hidaya katika kata ya Mvinjeni katikati ya mji wa Iringa.


 HILO NDILO BASI DOGO AINA YA HICE WALILOKUA WAKISAFIRIA LILOPINDUKA NA WAO KUNUSURIKA
ASKARI POLISI NA WASAMARIA WEMA WAKIWAOKOAWATOTO WALIONUSURIKA KATIKA AJALI HIYO
 WANANCHI WAKISHUHUDIA GARI LILILOPATA AJALI LIKIWA NA WATOTO 25 WA SHULE YA ST.CHARLES

 WATOTO WALIONUSURIKA WAKILIA KWA UCHUNGU WAKIWAHITAJI WAZAZI WAO.
WATOTO WALIONUSURIKA KATIKA AJALI HIYO WAKIINGIZWA  KWENYE GARI KUPELEKWA HOSPITALI KWAAJILI YA KUANGALIWA AFYA ZAO ZAIDI

 ASKARI POLISI AKICHUKUA MAELEZO KWA WATOTO WALIONUSURIKA AJALINI
WATOTO WALIONUSURIKA KATIKA AJALI WAKISUBIRI HUDUMA HOSPITALINI
 ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WAKIKAKUA GARI LILILOPATA AJALI LIKIWA NA WATOTO 25
 WANANCHI WAKISHANGAA AJALI

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!