WAZIRI MKUU WA UBELGIJI AMCHOKOZA OBAMA KOMBE LA DUNIA.
Home
»
Unlabelled
» WAZIRI MKUU WA UBELGIJI AMCHOKOZA OBAMA KOMBE LA DUNIA.
Waziri mkuu wa Ubelgiji Elio Di Rupo amemtumia ujumbe raisi wa marekani Barack Obama wa utani baada ya kujigamba kwamba usiku wa leo Ubelgiji itawafunga Marekani na kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia huko nchini Brazili.
Hata hivyo pamoja na vijigambo hivyo vya waziri mkuu wa Ubelgiji Raisi wa Marekani Barack Obama hakutaka kujibu lolote ikiwa ni kama ishara ya kusubiri matokeo ya mtanange huo.
Siku ambayo Raisi wa Marekani Barack Obama alipoishuhudia kwenye ndege timu yake ya taifa ikiambulia kipigo kutoka kwa Ujerumani.
Obama akiwa na mshauri wake ndani ya Air Force One wakiishuhudia timu ya taifa ya Marekani ikipambana na Ujerumani na kuambulia kipigo.
Huu ndio ujumbe wa waziri mkuu wa Ubelgiji kwa Raisi wa Marekani Barack Obama kwenye ukurasa wake wa tweet.
0 comments:
Chapisha Maoni