Searching...
Jumatano, 2 Julai 2014

CHELSEA YAING'OA MAREKANI KOMBE LA DUNIA




Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji na mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Kevin De Bruyne akipiga mpira uliotinga kimiani moja kwa moja na huku mabeki wa Marekani wakijitahidi kumkaba bila mafanikio.
Kiungo mshambuliaji huyo De Bruyne akiwanyanyua mashabiki wa Ubelgiji baada ya kufunga goli safi dakika za nyongeza.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji wakimpongeza De Bruyne baada ya kazi zuri na kuihakikishia Ubelgiji kutinga hatua ya robo fainali kombe la dunia linaloendelea huko nhini Brazili.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji na klabu ya Chelsea Romelu Lukaku akiifungia timu yake goli la pili ambalo liliizamisha kabisa Marekani na kuzima ndoto za vijana wa Obama kutinga robo fainali ya mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea huko nchini Brazili.
Delight and despair: Belgium players celebrate with Lukaku as Howard reacts to conceding Belgium's second
Wachezaji wa Ubelgiji wakimpongeza Romelu Lukaku baada ya kufunga goli la pili.
Dejected: Howard looks to the ground after conceding but kept USA in the game for much of the tie
Mlinda mlango wa Marekani Tim Howard akiwa hoi baada ya kuchambuliwa magoli mawili ya haraka haraka na kupoteza matumaini ya kusonga mbele.
Great technique: Bayern Munich youngster Julian Green scores for America as Toby Alderweireld watches on
Mchezaji kinda wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Marekani aliiweka roho juu Ubelgiji baada ya kufunga goli safi dakika kumi kabla ya mechi kumalizika ambapo mechi hiyo ilikwenda dakika 120 baada ya kumaliza dakika 90 wakiwa suluhu ya bila kwa bila.



0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!