ARSENE WENGER.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema yupo mbioni kumsajili ,mlinda mlango namba mbili wa Real Madrid Iker Casillas kufuatia kocha wa Arsenal kuendelea kutafuta mlinda mlango namba moja kunako dimba la Emirates.
Kufuatia taarifa kutoka Hispania katika gazeti la Mundo Deportivo, zinasema Wenger amempigia simu Casilas kumshawishi kujiunga na Arsenal na huenda Wenger akafanikiwa mpango wake huo kufuatia mlinda mlango huyo kusugua benji huku akimshuhudia Diego Lopez akianza japo bado kocha wa Madrid Carlo Ancelotti ana matumaini makubwa sana na Casillas.
0 comments:
Chapisha Maoni