UFARANSA NJE KOMBE LA DUNIA,UJERUMANI HAOOOOOOOOOO NUSU FAINALI.
Home
»
Unlabelled
» UFARANSA NJE KOMBE LA DUNIA,UJERUMANI HAOOOOOOOOOO NUSU FAINALI.
Timu ya taifa ya Ujerumani imeifunga timu ya taifa ya Ufaransa kwa goli moja kwa sifuri na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa inayoendelea huko nchini Brazili.
Mchezaji wa beki wa Ujerumani Martin Hummels akiifungia timu yake goli pekee kunako dakika ya 12.
Mlinda mlango wa Ufaransa akichumpa kuokoa mchomo lakini anajikuta akiushuhudia mpira ukielea wavuni.
Hummels akishangilia goli lake pekee lililoivusha Ujerumani kwenda nusu fainali.
Umoja ni nguvu-wachezaji wa Ujerumani wakipongezana baada ya kuifunga Ufaransa.
Kiungo wa Hispania Yohan Cabaye akichuana na Benedikt Hoewedes wa Ujerumani.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ujerumani Thomas Muller akianguka ndani ya eneo la hatari kutafuta penalti lakini mwamuzi alimpuuza na kuendelea na game.f
beki wa Ufaransa Patrice Evra na golikipa wake wakiwa chini kuokoa mchomo wa mchezaji wa Ujerumani.
Mshambuliaji wa Ujerumani Miroslav Klose akichuana vilivyo na Mathieu Debuch.
Mlinda mlango wa Ujerumani Manuel Neuer akiokoa shuti kali kutoka kwa Mathieu Valbuena wa Ufaransa.
Kiungo wa Ujerumani Toni Kroos akipambana na Paul Pogba
beki wa Ujerumani Varane akiokoa mchomo.
Mshambuliaji wa Ujerumani Karim Benzema akihangaika kusawazisha goli bila mafanikio.
Blaise Matuidi wa Ufaransa akichuana na Bastian Schweinsteiger huku Jerome Boateng akiwa karibu kabisa kutoa msaada.
Kiungo wa Ujerumani Sami Khedira akilimwa kadi ya njano baada ya kufanya madhambi uwanjani.
0 comments:
Chapisha Maoni