Nyota
wa timu ya soka ya Brazil na kipenzi cha Wabrazili Neymar hatoshiriki
tena katika michuano ya kombe la dunia baada kupata jeraha katika mchezo kati ya Brazili na Columbia,mchezo ambao walishinda 2-1
Kipenzi cha wabrazili Neymar akitolewa nje kwa machela ikiwa ni dakika tano tu kabla mpira kumalizika kitendo ambacho kimewachanganya na kuwasononesha mashabiki,viongozi na wachezaji wenzake wa Brazili.
Taarifa
ya Daktari wa Brazili zinasemaMfupa wake unaoshikana na uti wa mgongo
ilivunjika katika mechi ya ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Colombia.
Hiyo ni picha ya X-ray ikionyesha mfupa wake wa uti wa mgongo uliovunjika.
Ni masikitiko makubwa kwa Brazili kumkosa nyota wao kwenye fainali dhidi ya Ujerumani lakini kwa hakika ni taarifa njema kwa Wajerumani kwani ni moja ya ahueni kwao kutinga fainali.
Mashabiki wa timu ya Brazil wakiwa nje ya hosiptali ya Sao Carlos Hospital ambapo kipenzi chao kimelazwa wakisubiri majibu ya daktari.
Jinsi muda ulivyokua unakwenda ndivyo mashabiki walizidi kuongezeka nje ya hosiptali hiyo kama wanavyoonekana hapo juu.
Ukiachilia mbali Brazil kumkosa Neymar nusu fainali dhidi ya Ujerumani lakini pia itaendelea kushiriki katika
mashindano hayo bila nahodha wake Thiago Silva katika mchuano wa nusu
fainali dhidi ya Ujerumani baada ya mchezaji huyo kupewa kadi ya pili ya
Njano.
Neymar akipatiwa Huduma ya kwanza,huku akiugulia maumivu makali.
0 comments:
Chapisha Maoni