Mahost wa Show ya Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwa kwa Steji tayari kwa Show kuanza.… 
Timu
ya Tanzania Movie Talents (TMT) ikiwa katika maandalizi ya mwisho
mwisho kabla ya Show ya Tanzania Movie Talents katika ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa usiku wa kuamkia leo. 
Baadhi
ya wakazi wa jiji la Dar waliohudhuria kwaajili ya kutazama onyesho la
washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT)
linaloendelea kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa. 
Wadau waliojitokeza kwaajili ya Kushuhudia onyesho la Tanzania Movie Talents.
Washiriki 20 wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni
washindi kutoka kanda 6 za Tanzania wamepanda kwa steji katika ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa kwaajili ya kuanza kuonyesha vipaji vyao vya
kuigiza. Sasa ni safari kwa washiriki kuelekea kwenye kinyanganyiro cha
kuwania Milioni 50 za Kitanzania katika fainali kubwa itakayofanyika
Mwisho wa Mwezi wa Nane.
Katika Onyesho hili litakalorushwa katika Runinga ya ITV siku
ya Jumamosi saa 4 usiku kitakuwa kipindi cha kwanza kwa watanzania
kuanza kuangalia na kuwapigia kura washiriki ambao watakuwa wamewavutia
na kukonga nyoyo zao na hatimaye kuwawezesha kushiriki katika fainali
kubwa Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
Watanzania wanatakiwa kuendelea kutazama muendelezo wa vipindi
vya TMT kupitia Kituo cha Runinga cha ITV saa nne Usiku siku ya
Jumamosi na hatimaye kuanza kuwapigia kura washiriki. Ili kuweza kupata
Taarifa za TMT unaweza kutuma neno "TMT" kwenda namba 15678
Mchujo kwa washiriki sasa waanza rasmi ili kuweza kumpigia
kura mshiriki umpendae unatakiwa kutuma neno "TMT ikifuatiwa na namba ya
Mshiriki" kwenda namba 15678
Picha/Habari na Josephat Lukaza - Proin Promotions - Dar Es Salaam.
0 comments:
Chapisha Maoni