
Liverpool wameingilia kati kumnasa Baloteli ambapo kocha wa Liverpool Rodgers anaamini kuwa Baloteli ndio mbadala wa Suarez Liverpool,ambapo Suarez anaelekea kutua Barcelona kwa kitita cha paundi milioni 80.Wakala wa Balotelli Mino Raiola, amesema mtukutu Baloteli amesema hataki kucheza ligi yoyote ile tofauti na ya England.
Kocha wa Arsenal Arsenal Wenger amekua akilaumiwa kwa kufanya makosa ya wazi hasa pale wachezaji wanapoweka wazi wenyewe kwamba wanataka kucheza Arsenal lakini yeye anawapuuza na hatimaye kunyakuliwa na vilabu pinzani,nahodha wa zamani wa Arsenal Cesc Fabregas alimpigia simu Wenger kwamba anataka kujiunga na klabu yake ya zamani lakini Wenger alimpuuza na baadaye akanaswa na Chelsea.
Mchezaji mwingine ambaye amesema anataka kujinga na Arsenal ni Alexis Sanchez lakini hadi sasa Wenger anaonekana amelala usingizi wa Pono huku mchezaji huyo akimezewa mate na Liverpool,Chelsea,Man U,Real Madrid na Inter Millan.
0 comments:
Chapisha Maoni