Siku chache kabla ya kocha mpya wa Manchester United Louis Van Gaal kutua rasmi OT kukianza kibarua chake, tayari ameshaanza makeke ukiachilia mbali ya usajili lakini sasa amewataka maofisa wa Manchester United kumuuza hara kiungo wa Ubelgiji Marouane Fellaini bila kujali kitita kilichotumika kumnunulia kutoka Everton cha paundi milioni 27.
Akizungumza kutoka nchini Brazili ambako anakiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi kwenye mnyukano wa vigogo vya soka kugombea kombe la dunia, Van Gaal amesema amekua akimfuatilia kwa karibu sana Fellaini lakini hajaridhishwa na kiwango chake hata kidogo kwahiyo ameagiza aondoke maana hayupo kwenye mipango yake msimu ujao.
0 comments:
Chapisha Maoni