Hivi ndivyo hali ilivyokua huki nchini
Brazil ambapo maelfu ya washabiki wa timu ya taifa ya Brazili
walijikusanya kwenye beach Copacabana beach huko Rio de Janeiro
kushuhudia meche ya kihistoria kati ya wababe Brazili dhidi ya Chile.
Mechi ambayo imechukuliwa kama fainali ambapo Brazili walishinda kwa
penalti 3-2 baada ya kumaliza dakika 120 wakiwa sare ya bao 1-1
Hivi ndivyo hali ilivyokua huko katika beach ya Copacabana na hapa hali ilikua tete zaidi kwani ndio ilikua wakati wa mikwaju ya penalti,hivyo beach ilikua kuna wakati kunakua kimya kama hakuna watu na Brazili wakifunga ni kelele mithili ya ndege boeng 777 ikitua uwanjani.
Baadhi ya mashabiki wa Brazili wakishangilia ushindi wa kutinga robo fainali ya michuano hiyo ya kombe la dunia huku mmoja akiwa amevalia kinyago cha Suarez mlawa watu.
Mwanadada wa Brazili akicheza samba muda mfupi kabla ya mechi kati ya Brazili na Chile.
Hivi ndivyo hali ilivyokua katika beach ya Copa Cabana Rio De Janeiro wakati wa mechi kati ya Brazili na Chile ambapo Chile walitolewa kwa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya kumalizika kwa dakika 120 wakiwa sare ya bao 1-1
TAFADHALI SHARE HABARI ZOTE ZA MCHOME BLOG ILI MARAFIKI ZAKO PIA WAZIONE.
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.