Uwanja wa Maracana uliopo jijini Rio De Janeiro ukiwa umefurika maelfu ya mashabiki wa Uruguay na Columbia,huu uwanja ulijengwa mwaka 1950 na una uwezo wa kuchukua watazamaji 74,738 wote wakiwa wamekaa na leo hii uwanja huu ndio utaamua nani kati ya Uruguay na Columbia kutinga hatua ya robo fainali kumfuata Brazili ambaye amemtoa kwa penalti Chile baada ya dakika 120 za mtanange kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mchezaji wa Columbia Rodrguez akifunga goli bora ambalo linashindana na goli la Van Persie,na wataalamu wa soka wanasema huenda hili likawa bora zaidi kuliko la Van Persie.
Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani akimlalamikia mwamuzi baada ya kuwapa Columbia free kick yeye akidai kwamba sio halali.
Shabiki wa Columbia akiwa ameshika bango linalouliza "yuko wapi Suarez?"
Mashabuiki wa Uruguay wakiwa wamebeba vinyago vya sura ya Suarez katika mechi kati ya Uruguay na Columbia ambapo Uruguay walichabangwa mabao 2-0 huku pengo la Suarz likionekana wazi kabisa.
0 comments:
Chapisha Maoni