Nchi nzima ya Brazili imezizima baada ya dakika 120 za mtanange mkali kati ya miamba ya soka ya Amerika ya Kusini Brazili na Chile kumalizika kwa wenyeji Brazili kuibuka na ushindi wa penalti 3-2 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na mlinda mlango wa Brazili Julio Cezar baada ya kuokoa mikwaju miwili ya Penalti.
Mashabiki wa Brazili wakishangilia kwa nguvu huku wakiwa hawaamini macho yao na masikio yao kama wametinga robo fainali.
Wachezaji wa Brazili wakishangilia ushindi baada ya mchezaji wa Chile kukosa penalti
Haooooooooooooooo Robo fainali.
David Luiz akifurahia ushindi baada ya Chile kukosa mkwaju wao wa Penalti ambao umewapa tiketi ya kucheza robo fainali.
Brazili hawakuamini macho hadi kufikia kutoa machozi ya furaha.
Brazili hawakuamini macho hadi kufikia kutoa machozi ya furaha.
Hali ilikua tete sana kwa Chile baada ya kukosa huo mkwaju wa penalti.
...Hakuna presha mbaya katika soka kama inapofika wakati wa kuamua mshindi kwa penalti.
Mchezaji wa Chile akipiga penalti ambayo iligonga mwamba na kurudi uwanjani na kuipa tiketi Brazili kutinga robo fainali ya kombe la dunia nchini Brazili baada ya kazi nzuri waliyoifanya dakiak 120 na kutoka sare ya 1-1.
Wachezaji wa Brazili wakimpongeza mlinda mlango wao Julio cezar baada ya kuokoa mkwaju wa kwanza wa penalti kutoka kwa Chile.
Beki wa Brazili David Luiz akishangilia goli lake la penalti dhidi ya Chile.
Umoja ni nguvu,baada ya dakika 120 sasa wabrazili wanakumbatiana kutiana moyo kuelekea kwenye mikwaju ya Penalti.
Baada ya dakika 90 za maumivu sasa vijana wanajipanga kwa dakika 120 ili kutafuta mshindi wa kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la dunia 2014.
Mpambano ulikua siio mchezo ndani ya dakika 120, huyo hapo juu ni msukuma ndinga wa Chile akigangwa baada ya kupata mshike mshike uwanjani.
0 comments:
Chapisha Maoni