Mchezaji nyota na kipenzi cha Wabrazil Neymar akishangilia goli lake la pili katika mechi kati yao na Cameroon na kuihakikishia Brazil kutinga hatua ya kumi na sita bora, katika mchezo huo Cameroon ililala kwa jumla ya mabao 4-1

Neymar akitumbukiza mpira kimiani baada ya kuwalamba chenga mabeki wawili wa Cameroon.

Dani Alves na David Luiz wakimpongeza Neymar huku Neymar akisikiliza makelele ya furaha ya mashabiki wa Brazili ambao walikua wamefurika uwanja mzima.
Neymar alikua mwiba mkali kwa wacameroon

Raha ya ushindi kushangilia.

Mchezaji wa Cameroon Joel Matip akishangilia goli lake aliloifungia timu yake dhidi ya Brazil.

Wacameroon walishangilia sana waliposawazisha goli lao lakini furaha yao ilidumu kwa muda mfupi sana.

Goooooooooooooooool

Mshambuliaji wa Brazil Fred (9) akizima furaha ya Wacameroon baada ya kufunga goli la tatu na kufanya ubao kusomeka 3-1.

Kipenzi cha wabrazil Neymar alilazimika kutolewa uwanjani dakika ya 71 baada ya kuumia goti

Beki kisiki wa Brazil David Luiz akishangilia kutinga hatua ya 16 bora.

Beki wa Brazil Marcelo akilalamika baada ya kuchezewa ndivyo sivyo na mchezaji wa Cameroon.

Nyota wa Brazil na Barcelona akifanya yake uwanjani

Mshambuliaji wa Cameroon Benjamin Moukandjo akipambana na wachezaji wa Brazil Neymar na Mercelo

Kiungo mkabaji wa Cameroon Enoh Eyong akianguka baada ya kuzidiwa ujanja na mchezaji nyota wa Chelsea Oscar.
0 comments:
Chapisha Maoni