Katika kipindi chote cha kampeni, vyama vitano vilichuana kumwaga
sera na usiku na mchana katika Kata 15 za jimbo hilo, kila kimoja
kikiamini ndicho kitaibuka mshindi na hatimaye kutoa mrithi wa
Bwanamdogo.
Vyama hivyo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachowakilishwa na
Ridhiwani Kikwete, Chadema ambacho mwakilishi wake ni Mathayo Torongey
na Chama cha Wananchi (CUF) kinachowakilishwa na Fabian Skauti.
Vingine ni AFP ambacho mpeperusha bendera wake ni Ramadhani Mgaya na NRA kinachowakilishwa na Munir Hussein.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Chalinze ambaye pia
ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Christina Njovu,
maandalizi yote ya uchaguzi huo mdogo yamekamilika.
Alimwambia mwandishi jana kuwa, Jimbo la Chalinze lina vituo vya
kupigia kura 288 ambavyo pia vilitumika katika uchaguzi wa mwaka 2010 na
kwamba wasimamizi wa uchaguzi wako tayari kwa kazi hiyo, huku
akisisitiza waliojiandikisha na kutambuliwa katika daftari la wapiga
kura katika jimbo hilo ni wapiga kura 92,588.
Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei amesema na
kutahadharisha wananchi watakaopiga kura kufanya hivyo na baadaye
kuondoka eneo la kupiga kura umbali wa zaidi ya meta 100.
Alisema kazi ya ulinzi na usalama katika vituo vyote ni kazi ya jeshi
la polisi na sio mtu ama kikundi chochote kiwe cha siasa ama sio cha
siasa na iwapo hilo litazingatiwa uwezekano wa upigaji kura na
utangazaji matokeo ukawa wa amani na utulivu.
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.