 |
Mstahiki
meya wa manispaa ya Shinyanga mheshimiwa Gulam Hafiz Mukadam akishikana
mkono na aliyekuwa diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya
Shinyanga bwana Sebastian Peter Mzuka maarufu kama Obama wa Ngokolo muda
mucha baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama ya Mwanzo mjini
Shinyanga katika mkutano wa katibu wa siasa na uenezi wa ccm taifa Nape
Nnauye mkutano ambao wananchi wameouona kama ulikuwa na nia ya kuwapokea
viongozi wa chadema Sebastiani Peter na Zacharia Mfuko wa kata ya
Masekelo ambao kwa pamoja jana walifanya maamuzi ya kujivua udiwani wa
kupitia tiketi ya CHADEMA. | |
|
 |
Waliokuwa
madiwani wa CHADEMA,kulia ni Sebastian Peter,aliyekuwa diwani wa
Ngokolo katikati ni Nape Nnauye na kulia ni Zacharia Mfuko aliyekuwa
diwani wa Chadema kata ya Masekelo wakiwa juu ya jukwaa kabla ya kuvua
magwanda na kurudisha kadi zao na kujiunga na CCM mbele ya Nape Nnauye
jioni ya leo mjini Shinyanga |
 |
Mapema
wakati wa mkutano wa hadhara wa Chama cha mapinduzi CCM jioni ya
leo,Katibu wa siasa na uenezi CCM taifa Nape Nnauye akizungumza katika
mkutano wa hadhara mjini Shinyanga katika viwanja vya mahakama ya mwanzo
eneo la Nguzo Nane mjini Shinyanga.Kushoto ni mbunge wa jimbo la
Shinyanga mjini,ambaye pia ni naibu waziri wa madini Stephen Masele.
 |
Aliyekuwa diwani wa Chadema Zacharia Mfuko juu ya jukwaa la CCM kama unavyoona amevaa mali za CCM |
|
 |
Aliyekuwa
diwani wa Chadema katika kata ya Ngokolo Sebastian Peter akizungumza
katika mkutano wa CCM leo ambapo alisema ameamua kujiunga/kurudi
nyumbani kwa hiari yake bila kushinikizwa na mtu yeyote na kukanusha
habari zilizotapakaa mtaani kuwa yeye pamoja na mwenzake Zacharia Mfuko
wamehongwa shilingi milioni 15 ili wahamie CCM |
 |
Nguo za CHADEMA walizokuwa wamevaa Madiwani hao walizokuja nazo mkutanoni walivua na kuamua kuchoma moto |
 |
Ndani ya gari la CCM Sebastian Peter na Zacharia Mfuko wakiondoka eneo la mkutano wameshavaa nguo za CCM kama unavyoona |
 |
Wanachama hao wapya wa CCM,Ndiyo gari waliyoondoka nayo eneo la mkutano |
Kutoka
kushoto ni Zakaria Martin Mfuko aliyekuwa Diwani wa Kata ya
Masekelo(Chadema),na Kulia ni Sebastian Peter aliyekuwa diwani kata ya
Ingokole(Chadema) wakitambulishwa mbele ya umati wa watu na Katibu wa
NEC itikadi na uenezi Nape Nnauye kwenye viwanja vya Mahakama ya mwanzo
Shinyanga mjini ambao kwa moyo mmoja wamejiunga na CCM.
0 comments:
Chapisha Maoni