Searching...
Alhamisi, 6 Februari 2014

FISI WAFUKUA KABURI NA KUILA MIILI YA VIBAKA WALIOUAWA NA WANANCHI KWA KUCHOMWA MOTO WAKITUHUMIWA KWA WIZI


Katika hali isiyokuwa ya kawaida  wananchi wa kijiji cha Iponya kata ya Kagongwa Wilayani Kahama Mkoani Shinyinga wamelazimika kuzika upya mabaki ya Marehemu wawili waliozikwa wiki iliyopita baada ya leo kukuta wamefukuliwa  na Fisi.

Miili hiyo ni ya  watu wawili ambao  walisadikiwa kuwa vibaka waliuwawa na wananchi  wenye hasira kali na kuchomwa moto na kisha kuzikwa katika makaburi yaliyopo katika kijiji hicho. 

Kwa mujibu wa mashuhuda wakizungumza  mwandishi wetu wamesema  hali hiyo imetokana na kuzikwa katika makaburi ambayo hayana kina kirefu hivyo wanyama hao kuwa rahisi kwao kufukua na kuanza kula maiti hizo....

Mmoja wa mashuhuda Hasan Msoma amesema  waligundua kutokana na wao kufika katika maeneo ya makaburi kwa lengo la kuzika Mtoto ndipo wakaona mabaki ya  miili ya marehemu  huku eneo kubwa  la miili ikiwa imeliwa na  fisi.

Amesema  baada ya kuona hali hiyo waliutaarifu uongozi wa kata  ambao ulifika na kushiriki katika mazishi na kusema kuwa haki za binadamu hazikuzingatiwa katika kuzika  watu hao kwani walifukiwa katika shimu lenye kina kifupi cha futi moja.

Hata hivyo viongozi wa kata hiyo hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kutokana na kutoonesha ushirikiano kwa mwandishi wetu.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!