Mchezaji bora wa dunia anayekipiga na klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Mess amehusishwa na kuhamia kati ya klabu ya Manchester City au PSG katika uhamisho wa dirisha dogo mwezi huu.
Lakini swali la walio wengi ni kwamba kwa klabu yoyote inayomuhitaji Mess itamgharimu paundi ngapi?
Mpaka sasa uhamisho ambao umeitikisa dunia ni ule wa Gareth Bale uliogharimu paundi milioni 85,ukifuatiwa na ule wa Christian Ronaldo wa paundi milioni 80 lakini kampuni moja ya kutathmini masuala ya thamani ya wachezaji ya Eurmericas imeweka wazi kwamba thamani halisi ya Mess ni paundi milioni 331
0 comments:
Chapisha Maoni