WAYNE ROONEY.
Hatimaye sasa matajiri wa Hispania maarufu kwa kuvunja Benk na kununua wachezaji ghali duniani Real Madrid sasa wapo katika mchakato wa kumnunua mshambuliaji wa kimataifa wa England ambaye pia anakipiga na Manchester United Wayne Rooney kwa kitita paundi 25 mwishoni mwa msimu huu atakapoingia katika mwaka wake wa mwisho na mkataba wake na Man U.
JUAN MATA.
Atletico Madrid wapo mbioni kuwazidi kete Manchester United katika kumsainisha kiungo mshambuliaji wa Chelsea Juan
Mata kwa kumtoa mshambuliaji wao Diego Costa, 25, pamoja na Brazilian beki wao wa kimataifa wa Brazil Filipe Luis, 28, ili tu wamuachie kiungo huyo wa Chelsea kutua Atletico Madrid.
JOLEON LESCOTT.
Imeelezwa kwamba beki wa kati wa Manchester City Joleon Lescott, 31, ataruhusiwa kuondoka klabuni hapo hata kabla ya msimu kumalizika endapo tu kocha wao Manuel Pellegrini atapata mbadala wake.
DANTE.
Beki wa Bayern Munich Dante, 30,amesema Manchester United wameonyesha nia ya kumsajili katika dirisha dogo la usajili mwaka huu.
LEE CATTERMOLE.
Timu ya Stoke City imesema imemalizana na klabu ya Sunderland kwa kumsajili kiungo wao Lee Cattermole, 25.kwa kitita cha paundi milioni 5.
THIBAUT COURTOIS.
Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone amesema wapo tayari kulipa kiasi chochote cha fedha ili kumbakisha mlinda mlango wa chelsea Thibaut Courtois, 21, anayechezea timu hiyo kwa mkopo ambapo huu ndio msimu wake wa mwisho kukipiga na klabu hiyo.
NIGEL DE JONG.
Liverpool wapo katika harakati za kumsajili kwa mkopo mchezaji wa AC Milan kiuongo Nigel de
Jong, 29, ili kuziba pengo la majeruhi Lucas Leiva.
LUIS NANI.
Sporting Lisbon wameingia katika vita vikali na Juventus katika kutafuta saini ya mshambuliaji wa pembeni wa Manchester United Luis Nani, 27 ili kumpa mechi nyingi zaidi kumuimarisha kabla ya kombe la dunia.
0 comments:
Chapisha Maoni