Msanii
wa Maigizo Tanzania Steve Mongere aka Steve Nyerere akisalimiana na
Mwendesha Kipindi cha The Mboni Show , Mboni Masimba (Wa Kwanza kushoto)
mara baada ya kuwasili ndani ya mjengo ambapo kipindi hiko hurekodiwa
Pembeni ni Msanii nguli wa Filamu Tanzania Elizabeth Michael "Lulu"
akifuatiwa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao
ni watengenezaji, wauzaji na wasambazaji wa Filamu za Kitanzania
Nchini.
Msanii
Nguli na mahiri aliye chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited
Elizabeth Michael "Lulu" akisikiliza kwa makini wakati msanii mwenzie
Steve Nyerere alipokuwa akiongea katika kipindi cha The Mboni Show
Mwendeshaji
wa Kipindi cha The Mboni Show Mboni Masimba (Wa Kwanza Kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na Muigiza Nguli katika tasnia ya filamu nchini
Elizabeth Michael aka Lulu aliye chini ya kampuni ya Proin Promotions
Limited mara baada ya kipindi kumalizika
Meneja
masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Evance Steven akiwa
tayari kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Mwendesha Kipindi Cha The
Mboni Show, Mboni Masimba wakati wa kurekodi kipindi hiko
kitakachorushwa leo Alhamisi
Muigiza
wa filamu za vichekesho Steve Mogere "Nyerere" akieleza mikakati yake
na filamu zake mpya alizotoa akiwa chini ya Kampuni ya Utengenezaji,
Usambazaji na Uuzaji wa Filamu za Kitanzania ya Proin Promotions Limited
wakati wa kipindi cha the Mboni Show kitakachorushwa hewani leo
Mboni
Masimba, mwendeshaji wa Kipindi cha the Mboni Show akimsikiliza Steve
Nyerere kwa umakini wakati msanii huyo wa vichekesho alipokuwa akielezea
Mikakati yake katika Mwaka huu na juu ya filamu zake alizozitoa akiwa
chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited
Mwendeshaji
wa kipindi cha the Mboni Show, Mboni Masimba (wa kwanza Kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni aliowaalika katika kipindi
chake cha The Mboni Show kitakachorushwa leo usiku. Kutoka Kulia Ni
Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited Evance Stephen, Msanii Nguli
na Mahiri Elizabeth Michael aka Lulu na Steve Mongere aka Steve
Nyerere.
Picha na Josephat Lukaza
0 comments:
Chapisha Maoni