WINGA wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard ameikataa ofa
ya Paris Saint-Germain ‘PSG’ ya Ufaransa na badala yake ameweka kuwa ataendelea
kuitumikia klabu yake ya Chelsea.
Hazard ametajwa kuwa ni mmoja wa wachezaji
wanaotakiwa na klabu ya PSG katika usajili wa dirisha dogo lakini nyota huyo
amefunguka na kusema kuwa hayuko tayari kwa sasa kuihama Chelsea.
Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji anasema Chelsea ndiyo
sehemu sahihi kwake kwa sasa kwani uwepo wake klabuni hapo kunampa nafasi zaidi
ya kujiendeleza kisoka.
0 comments:
Chapisha Maoni