Zitto Kabwe akiingia mahakama Kuu Dar es Salaam jana.
Wanasheria wa Chadema, Tundu Lisu (kushoto) na Peter Kibatala waliofika kupinga hoja hiyo mahakamani.
Tundu Lisu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakijadiliana jambo wakati wakisubiri uamuzi wa mahakama
Zitto na wakili wake Msando wakiwasiliana na marafiki zao walipokuwa
wakisubili uamuzi wa mahakama, ambapo Zitto aliibuka kidedea kwa pingamizi
lake kukubaliwa hivyo kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA iliyokuwa imepangwa kufanyika leo
kukatazwa kumjadili Zitto kwa namna yoyote ile.
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Zitto Kabwe (kulia) akitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania,
Dar es Salaam, ambapo aliwasilisha ombi la pingamizi la yeye
kujadiliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinachotarajia
kufanyika leo, hadi rufaa yake ya kupinga kuenguliwa wadhifa huo
kwenye Baraza Kuu la chama hicho. Kushoto ni Wakili wa Zitto, Albert
Msando. Mahakama Kuu imekubaliana na Zitto Kikao cha Kamati Kuu ya
Chadema kinachotarajiwa kufanyika leo kutomjadili kwa namna
yoyote ile.
0 comments:
Chapisha Maoni