Searching...
Ijumaa, 17 Januari 2014

NAIBU WAZIRI WA JK ABURUZWA MAHAKAMANI KWA KUKIUKA SHERIA

 
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Mheshimiwa Makongoro Mahanga.
Baadhi ya nakala za malada ya kesi hiyo iliyofunguliwa mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi na Bi. Itika Kasambala dhidi ya Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana.
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt Mahongoro Mahanga akitoka katika chumba cha mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi wiki iliyopita siku ya Jumanne baada ya kusomewa mashtaka yake ya kumfanyisha kazi PS wake (Private Secretary) Bi, Itika Kasambala katika ofisi yake ya Bunge kwa muda wa miaka kumi bila mkataba na kusitisha kazi yake na kisha kulipa mafao ya laki mbili tu
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana akishuka katika kazi za mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi wiki iliyopita siku ya Jumanne jijini Dar es Salaam.
 Bi. Itika Kasambala akiwa katika moja ya vyumba vya habari baada ya kufanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi
Bi Itika kasambala akiwa katika picha tofauti jijini Dar es Salaam baada ya kuelezea sakata lake na Naibu Waziri wa kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana
----
Na. Mwandishi wetu
NAIBU Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt Makongoro Mahanga ameingia kwenye kashfa nzito ya kuvunja sheria za kazi nchini kwa kumfanyisha kazi msaidizi wake (PS) wa ofisi yake ya Bunge kwa miaka kumi bila mkataba na kumlipa fedha taslimu shilingi laki mbili tu (200,000) kama mafao.
Naibu Waziri, Mahanga anakuwa kiongozi wa kwanza kuingia kwenye kashfa akiwa madarakani tena kwenye swala la ajira wakati yeye mwenyewe ni waziri mwenye dhamana na maswala ya ajira na haki za wafanyakazi nchini chanzo chetu kimeelezwa.
Kwa mujibu wa sheria za kazi na mahusiano kazini, Naibu Waziri amekiuka kifungu cha 3 cha sheria ya Taasisi za kazi za mwaka 2004 na pia amekiuka sehemu ya tatu ya viwango vya ajira na sehemu ndogo A kwa kushidwa kuandika mkataba kwa mujibu wa kifungu cha 14 ibara ya kwanza kama sheria ya kazi na mahusiano kazini inavyotaka.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!