Searching...
Jumapili, 26 Januari 2014

MASIKINI DIAMOND!!! CHIFU KIUMBE AMUUMBUA,KISA PRADO

Pedeshee Maarufu ajulikanae kwa jina la Chief kiumbe ameibuka na kuzua jambo kuwa lile Prado Diamond alilopiga nalo picha week kadhaa zilizopita na kusema ni gari yake mpya kuwa si ya Diamond bali ni Gari lake yeye..
Chief kiumbe Amesema haya hapa chini:
“Unajua mimi huwa sio mtu wa kuzungumza sana ila ukweli ni kwamba wasanii wengi wa hapa bongo wanatembelea magari yangu, na wala hawatoi hela yoyote,kwa mfano Diamond anamiliki gari yangu mpya ambalo nilinunua zaidi ya shilingi milioni 245 kipindi niko nje kiziara, nafanya hivi kwasababu ya upendo na pia wapo wasanii wengi tu, kuna wengine wanajitamba kwamba wamenunua ila sio kweli mimi ndio ninawapa bureee watembele hizo habari za kwamba wananunua hakuna kitu kama hicho,mimi napenda watu wafuate nyayo za Diamond naamini watafanikisha ndoto zao” – Kiumbe

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!