MAHAKAMA Kuu Kanda ya
Dar es Salaam, imeahirisha kutoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa jana na
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe (Chadema), kuhusu ombi la
kuitaka Mahakama hiyo kuizuia Kamati Kuu ya Chama hicho, kutomjadili
katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Chadema, wakitwangana nje ya Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam.
Mwanachama wa Chadema, anayepinga hoja za Zitto Kabwe, akimtwanga mfuasi wa Zitto Kabwe.
Hatua
hiyo ilisababisha Askari wa Jeshi la Polisi kuingilia kati, huku
wakiungana na upande wa Chadema na kuwatwanga marundi wafuasi wa Zitto
waliokuwa na mambango kama ilivyokuwa kwa wenzao wa Chadema.
Kesi
hiyo ilifunguliwa jana na wakili wa Mbunge huyo Albert Msando huku
wakili wa Chadema Tundu Lissu akiweka pingamizi,hata hivyo Jaji John
Utumwa wa Mahakama hiyo alitupilia mbali mapingamizi yote yaliyowekwa na
Tundu Lissu.
0 comments:
Chapisha Maoni