Pamoja na juhudi kubwa zilizofanywa na klabub ya Uturuki ya Trabzonspor kumsajili mshambuliaji anayeonekana kukosa namba Chelsea Demba Ba kwa paundi milioni 7,kocha wa Chelsea mreno Jose Mourinho amekataa kumuachia mshambuliaji huyo katika msimu huu baada ya mshambuliaji wake Fernando Torres kuumia.
‘Ukiachilia mbali kwamba Torres ameumia,lakini pia hatukuwa tayari kumuuza mshambuliaji wetu Demba Ba kama vyombo vya habari vinavyovumisha..bado tunamuhitaji sana Ba" alisema Mourinho.
Chelsea kwa sasa wanasubiria majibu ya vipimo vya scan vya goti la Torres,japokuwa tayari kuna tetesi kwamba huenda akawa nje ya dimba kwa muda wa wiki sita.
0 comments:
Chapisha Maoni