TUNDU LISSU-MWANASHERA MKUU WA CHADEMA.
Siku moja tu baada ya mahakama kuu ya Tanzania kukiamuru Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutojadili uanachama wa mbunge wa Kigoma Kaskazini mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe,mwanasheria mkuu wa CHADEMA ambaye pia ndiye mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni mheshimiwa Tundu Lissu ameiambia MCHOME BLOG kwamba chama hicho hakina mpango wowote wa kukata rufaa ya hukumu hiyo.
akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu Mheshimiwa Lissu amewataka wanachama wa CHADEMA nje na ndani ya nchi kutompatia ushirikiano wowote wa kichama kwani katiba ya chama hicho ipo wazi kwamba mwanachama yoyote anayekwenda mahakamani kukishtaki chama basi moja kwa moja anakosa uhalali wa kuwa Mwanachama wa Chama hicho kikuu cha upinzani hapa nchini.
MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI MHESHIMIWA ZITO KABWE.
jitihada za kumpata mbunge wa kigoma kaskazini mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe kuzungumzia kauli hiyo ya Mheshimiwa Lissu hazikuweza kuzaa matunda baada ya simu yake kutopatikana.
0 comments:
Chapisha Maoni