ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA,DR.WILLIAM MGIMWA.
Taarifa za kuaminika zilizotufikia hivi punde zinasema Waziri wa
fedha na uchumi mheshimiwa dr.William Mgimwa amefariki dunia leo asubuhi majira ya saa tano na dakika ishirini asubuhi katika hosiptali ya MEDICLINIC KLOFF huko
nchini Afrika Kusini alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
KATIBU MKUU KIONGOZI-BALOZI OMBENI SEFUE
Akizungumza na Mtandao huu katibu mkuu kiongozi
balozi Ombeni Sefue amesema taratibu za kuurudisha mwili wa marehemu hapa
nchini kwa maziko zinafanywa na ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini na hapo zitakapokamilika wananchi watajulishwa siku mwili wa marehemu utakapowasili.
Historia ya
William Augustao Mgimwa inaonyesha alizaliwa 20 January 1950 na alikua ni mbunge wa jimbo la Kalenga tangu mwaka 2010.
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU DR.WILLIAM MGIMWA MAHALA PEMA PEPONI AMINA.
0 comments:
Chapisha Maoni