ALIYEKUWA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII HAMIS KAGASHEKI.
ALIYEKUA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI DAVID MATHAYO DAVID.
Waziri
Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ametaka uthibitisho usio na shaka kwa
waliohusika wote na taasisi zao kuchunguzwa kiundani ili hatua stahiki
zichukuliwe. Kuendelea kulinda rasilimali na hifadhi za Taifa ameutaja
kuwa ni muhimu. Pia amesema ameongea na Waziri mmoja mmoja kuwa ni
busara ushauri wa wabunge utekelezwe. Amebainisha kuwa hata baada ya
kuongea na Rais. mkuu wa nchi ameridhia tume iundwe na kila aliyehusika
awajibike.
Amesema Rais ameshauri kutengua
uteuzi wa mawaziri wote wanne ( Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Wazir wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel
Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt David Mathayo, na
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki) kama ambavyo
wabunge walivyopendekeza.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe James Lembeli
(pichani juu) amesema kuwa kamati yake imeridhishwa na matokeo ya ripoti
ya kamati iliyosababisha hayo yote, na kwamba maelezo ya taarifa ya
kamati kimsingi yote yamekubalika.
Kuhusu
kumhusisha Dkt Mathayo ni kuwa Rais alishatoa maagizo tisa miongoni
likiwepo swala la kushughulikia wafugaji wanaohamahama. Amesema pia Rais
aliagiza pia kuwa wafugai wawe wa kisasa, pia kutafuta missing link ya
mifugo isipotee na pia kutafuta masoko nje ya nchi, ambapo amesema mengi
hayajatekelezwa.
Ameweka
bayana kuwa chimbuko kubwa ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, na
kwamba Waziri hakuwa anapewa taarifa za mara kwa mara.
Ameomba kipengele kiongezwe kuwa Katibu mkuu na watendaji wake wakuu waliohusika kuandaa Mpango kazi wa 'Operesheni Tokomeza' wawajibishwe.
Amesema rushwa iliyoko ndani ya wizara ya Maliasili na Utalii inatisha.
Spika amuomba Mwanasheria mkuu kutumia kifungu kuongeza muda. Naye ameomba kuundwa tume ya kisheria ya mahakama.
Juu ni Dkt Emmanuel Nchimbi aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani na chini ni Mhe Shamsa Vuai Nahodha aliyekuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa.
|
0 comments:
Chapisha Maoni