Searching...
Ijumaa, 20 Desemba 2013

MWENDESHA MASHTAKA ICC AOMBA KESI YA RAIS KENYATTA IAHIRISHWE .

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya Kimataifa mjini The Hague Fatou Bensouda amewaomba majaji wa mahakama hiyo kuiakhirisha kesi ya uhalifu dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kutokana na ukosefu wa ushahidi.
Bensouda amesema anahitaji muda zaidi ya kutafakari kesi hiyo baada ya shahidi mmoja muhimu kujiondowa na mwingine kukiri kutowa ushahidi wa uwongo. 
Kutokana na ombi hilo sasa majaji husika katika kesi hiyo wanabidi kutowa uamuzi wao wa ikiwa wataridhia kuichelewesha kesi hiyo au pengine kuitupilia mbali.Kesi ya Kenyatta inategemewa kuanza rasmi Februari

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!