RAIS JAKAYA KIKWETE
RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA Dr.
JAKAYA MRISHO KIKWETE LEO JUMATATU DESEMBA 30,2013 AMEMTEUA RASMI KAMISHNA WA
POLISI ERNESTI MANGU KUWA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI HAPA NCHINI.
TAARIFA ILIYOTOLEWA USIKU HUU NA KATIBU MKUU KIONGOZI,OMBENI
SEFUE INASEMA KUWA KAMISHNA ERNEST MANGU ANACHUKUA NAFASI YA MKUU WA JESHI HILO
LA POLISI HAPA NCHINI SAID MWEMA ANAYEMALIZA MUDA WAKE,UTEUZI WA KAMISHNA MANGU UNAANZA RASMI TAREHE MOSI JANUARY,201.
MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI NCHINI-KAMISHNA ERNEST MANGU.
KABLA YA UTEUZI HUO KAMISHNA MANGU ALIKUA MKURUGENZI WA ITELIJENSIA YA JINAI KATIKA JESHI HILO LA POLISI HAPA NCHINI.
AIDHA TAARIFA HIYO INASEMA KUWA RAIS KIKWETE AMEMTEUA KAMISHNA ABDULRAHAMAN KANIKI KUWA NAIBU MKUU WA JESHI LA POLISI ,NAFASI AMBAYO NI MPYA KATIKA MUUNDO WA SASA JESHI HILO HAPA NCHINI.
KABLA YA UTEUZI WAKE KAMISHNA KANIKI ALIKUA KAMISHNA WA UCHUNGUZI WA KIJINAI (COMMISSIONER FOR FORENSIC INVESTIGATIONS.
MKUU MPYA WA JESHI NA NAIBU WAKE WATAAPISHWA KESHO JUMANNE KATIKA VIWANJA VYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
0 comments:
Chapisha Maoni