Zitto Kabwe"Nimerudi nyumbani,Nawasshukuru kwa mapokezi mazuri haya ya Kihistoria hapa Kigoma,Nimerudi Shujaa wenu
Zitto"Asanteni sana,nawapenda sanaa"
Alipokuwa anakaribia kuingia Mwandinga Mh.Zitto kabwe alilazimika kuteremka na kuanza kutembea kuelekea kwenye Mkutano
Msafara bado unaendelea,Wananchi wanasema hakuna kurudi Nyuma mpaka kieleweke
Ni maelfu ya WANANCHI ambao wanatembea kuelekea Mwandinga umbali wa zaidi ya kilomita 15 kwa miguu huku wakiwa na furaha sana ya kukutana na Mbunge wao
Msafara wa magari zaidi ya 100 ukitokea Airpot kumpokea Mh.Zitto kabwe kuelekea Mwandinga,Hapa Shughuli za maendeleo zimesismama kwa muda wananchi wamejumuika kumsindikiza Zitto Mwandinga kuzumngumza na wanakigoma
Zitto Kabwe anasema"Nimerudi Nyumbani kuzungumza na nyini kaka,dada,baba na Mama zangu kuhusu maisha yangu ya Kisiasa,Nimerudi Nyumbani kwasababu ndipo nilipokulia na kuanza maisha,Pia nyie ndio mlionifikisha hapa".
Huu ni Upande mmoja wa Sehemu ya Mkutano wananchi wakiwa makini kusikiliza kile Mh.Zitto anaongea kuhusu mwenendo wa Siasa za CHADEMA na namna atakavyokuwa wamwisho kuondoka CHADEMA kwa hiari yake.
Msafara ukiendelea zaidi ya Kilomita 15 kutoa Airport Kuelekea Mwandinga Nyumbani alikozaliwa Zitto Kabwe,Wananchi wamejitokeza kwa wingi sana haijawahi kutokea.
Mh.Zitto Kabwe akaihutubia Maelfu ya Wananchi katika viwanja vya Mandinga,Kubwa amesisitiza ataendelea kudai Demokrasia ya Kweli ndani ya CHADEMA na inamuuma sana kuona wanaompiga Mishale ni Wanachadema wenzake.
Maelfu ya Wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano wa Mh.Zitto kabwe hapa Mwandinga Kijijini kwake alikozaliwa Mkoani Kigoma,Bango linasomeka "ZITTO KAMA MANDELA KASORO JELA"
PICHA KWA HISANI YA JAMII FORUM
0 comments:
Chapisha Maoni