Mmoja kati ya mbeki bora wakushoto duniani Ashley Cole wa chelsea anatarajiwa kusugua benji jumatatu pale timu yake ya Chelsea watakapo shuka dimbani kuvaana na vinara wa ligi kuu England Arsenal baada ya kufumwa na mapaparazi na kupigwa picha akisherehekea sikukuu ya Xmass na nyota kadhaa wa Arsenal.
akizungumzia sakata hilo kocha wa klabu hiyo ya Chelsea Mreno Jose Mourinho amesema maisha ya mchezaji binafsi hayamuhusu lakini akasisitiza kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa England Ashley Cole atashuhudia mpambano wa vigogo hao Chelsea na Arsenal akiwa jukwaani.
‘ilikua ni siku huru kwao, mimi sio baba yao, mimi ni kocha, na siwezi kuwalinda kwa kila kitu wanachokifanya pale wanapokuwa nje ya kambi.
‘sihitaji kuchangia lolote katika hili, nina maoni yangu, na sio tu kwa Ashley Cole..lakini acha iwe Historia...alisema Mourinho.
‘ninatarajia kumchezesha Branislav Ivanovic kama beki wa kulia,Cesar Azpilicueta beki wa kushoto. John Terry atacheza kama beki wa kati, na hapo sasa nitaamua kati ya Gary Cahill na David Luiz.Mourinho aliweka wazi silaha zake.
ikumbukwe kwamba Cole hajawahi kupewa kipaumbele katika ligi kuu England tangu Chelsea walipofungwa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle mapema mwezi wa kumi na moja mwaka huu.
0 comments:
Chapisha Maoni