Afisa Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa
(UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungmza na wanafunzi wa shule ya
Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro juu ya umuhimu wa kujihusisha na kazi
za Umoja wa Mataifa wakati wa ziara za kutembelea shule mbalimbali za
mkoa huo.
Na. Mwandishi wetu.
Vijana wa shule za sekondari nchini
wameaswa kuwa mabalozi wazuri pindi watakapomaliza masomo yao juu ya
kuhamasisha utekelezaji wa malengo ya milenia kwa sababu ni dira ya
maendelo ya taifa na dunia kwa ujumla.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya
Wasichana Kibosho, Lyamungo na Umbwe sekondari hivi karibuni, Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, Bi. Usia Nkhoma Ledama
amesema malengo ya milenia yanagusa Nyanja zote za maendelo kwa vijana
walio na wasio mashuleni.
Bi. Nkhoma amewataka wanafunzi wafanye
kazi za kujitolea na kuhakikisha wanapeleka elimu waliopata kupitia
vilabu vya Umoja wa Mataifa kwa jamii na kuhamasisha dhana ya kujitolea
kwa maslahi ya nchi.
“kila ndani ya saa moja tuna vijana 50
ambao wanapata maambukizi ya VVU kati ya miaka 14-24 ambao wengi kati
ya hao ni Wasichana, hivyo msijihusishe na masuala ya mapenzi mnapokuwa
mashuleni”, amesema Bi. Nkhoma.
Bi. Usia Nkhoma Ledama akionyesha
takwimu za Mimba za Utotoni zilizotolewa hivi karibuni (“Young People
Today. Time to Act Now”) ambapo asilimia 25 ya watoto wa kike chini ya
miaka 14 wanapata wakiwa mashuleni.
Pichani juu na chini ni vijana wa shule
ya Sekondari Umbwe wakifuatilia kwa umakini mjadala wa masuala ya Umoja
wa Mataifa uliiongozwa na Bi. Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani).
Mwenyekiti Taifa wa Vilabu vya Umoja wa
Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw. Rahim Rajab Nasser
akifafanua jambo kwa vijana waliojiunga na klabu za Umoja wa Mataifa
shuleni hapo juu ya umuhimu wa kuwa na cheti cha klabu ya Umoja wa
Mataifa
Msafara wa wajumbe wa kituo cha Habari
cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja
wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakitazama baadhi ya kazi mbalimbali
zinazofanywa na klabu ya Umoja wa Mataifa katika shule ya sekondari
Umbwe ikiwemo shughuli za kuchangia damu, kusafisha mazingira na
mengineyo yajihusishayo moja kwa moja na shughuli za jamii.
"Ubovu wa miundombinu ni changamoto
kubwa kwa ziara yetu lakini ujumbe wa shughuli za Umoja wa Mataifa
lazima ziwafikie walengwa".
Afisa Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa
(UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifurahia uwepo wake mbele ya wanafunzi
wa Kibosho Girls shule ambayo binafsi alisoma miaka 20 iliyopita,
ambapo pia ujio wake ulikuwa chachu na hamasa kubwa kwa wanafunzi wa
shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Wasichana Kibosho wakimsikiliza kwa makini Bi. Usia Nkhoma Ledama.
Afisa Habari wa Kituo cha Umoja
Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akiwasisitizia wasichana wa shule
ya Kibosho juu ya umuhimu wa kujiamini na kujitambua wakati wa maamuzi
yao binafsi.
Mmoja wa wanafunzi akiuliza swali kwa wajumbe wa Umoja wa Mataifa.
0 comments:
Chapisha Maoni