MJUMBE
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini na mhadhiri mwandamzi wa Sheria
wa Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB), Dk. Sengondo Adrian Mvungi, saa saba
usiku wa kuamkia siku ya jumapili amevamiwa
na watu wasiyojulikana nyumbani kwake Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar
es Salaam na kumcharanga mapanga maeneo ya mwilini mwake ikiwemo sehemu
za kichwani kwa madai kuwa watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi
walikuwa wakimshinikiza awapatie fedha na Dk. Mvungi alipowaambia hana
fedha ndipo walipoanza kumcharanga mapanga.
Mtoto
mkubwa wa Dk. Mvungi, Dk. Natujwa Mvungi ambaye ni Mkuu wa Shule ya
Sheria ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es Salaam, saa nane usiku
alimdhibitishia mwandishi wa habari hizi kuwa ni kweli baba yake ambaye
aliwahi kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, lakini
kura kwa upande wake hazikutosha na hatimaye aliyekuwa mgombea mwenzie
kwa tiketi ya CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ndiye aliyeshinda na
kutangazwa kuwa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi sasa
alivamiwa na kujeruhiwa na mapanga na watu wasiyojulikana.
Dk.
Natujwa anasema baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa
kuondoka, walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani
Pwani, na kupatiwa matibabu ya huduma ya kwanza na kisha kumkimbiza
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alisema kwanza alipokelewa
katika eneo la Emergence na kisha saa kumi na moja asubuhi aliingizwa
kwenye wodi ya Taasisi ya Mifupa Moi kwa ajili ya kuanza kupewa
matibabu.
Habari na Hapiness Katabazi
0 comments:
Chapisha Maoni