Searching...
Jumamosi, 16 Novemba 2013

MAOFISA WA TRA WANAOTUHUMIWA KUHUSIKA NA UJANGILI WA MENO YA TEMBO HAWA HAPA.

 
KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR-CP MUSSA ALI MUSSA.
MussaBalozi Kagasheki akiwa visiwani Zanzibar katika zoezi la kupakuwa shehena kubwa ya pembe za Tembo zilizokamatwa ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915 ambayo haijawahi kukamatwa nchini, alisema kwamba TRA wanahusika katika ujangili huo kwa sababu wao ndiyo wenye mamlaka ya kuhakikisha kwamba mizigo yote haramu haipiti katika bandari hiyo.
"Katika hili siwezi kumumunya maneno, lazima tu niseme ukweli hata kama wenzetu hawa watakasirika, lakini ukweli ni kwamba hawana pa kukwepea kwani wanahusika kwa asilimia 100 katika ujangili huu, kwa sababu kama watu wasingekuwa na maslahi katika hili kontena lisingekamatiwa hapa Zanzibar, hii ni ishara kwamba TRA wanahusika na kusaidia kulipitisha hadi huku," alisema Balozi Kagasheki.
Balozi alisema kwamba, shehena hiyo iliyokuwa tayari kusafirishwa kuelekea Philiphine ilikuwa katika magunia 98 yaliyochanganywa na magunia mengine ambayo yalikuwa yamefungwa pamoja na baadhi ya vitu vya baharini yalikuwa tayari yameshawekwa ndani ya kontena la futi 40 tayari kwa kusafirishwa kwenda Philiphne yakiwa katika hatua za mwisho za mamlaka husika za bandarini.
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi Zanzibar limewakamata watuhumiwa wengine watatu wakiwemo Maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA kituo cha Bandari Zanzibar kwa kuhusika na kashfa ya kupatikana kwa meno ya tembo yenye thamani ya Mabilioni ya shilingi.
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amewataja Maafisa hao wa TRA waliokamatwa kuwa ni Omari Hamad Ali(50) na Mohammed Hija(48) ambao wote wanafanyia kazi katika Bandari ya Zanzibar. Mtuhumiwa mwingine ni kibarua wa Mamlaka ya bandari Zanzibar Haidar Ahmad Abdallah(54).
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunaifanya idadi ya watuhumiwa waliokamatwa hadi sasa kwa kuhusika na sakata hilo kufikia watano.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!