Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari
ya kata ya Mgomba pamoja na walimu wao,Katibu Mkuu alitembelea shuleni
hapo kuona utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya maabara .
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaidiana na fundi katika kukamilisha
hatua za mwisho za upigaji lipu wa wa jengo la maabara la shule ya
Sekondari ya kata ya Mgomba iliyopo wilayani Tunduru.
Katibu wa NEC
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa kwenye picha ya
pamoja na wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari ya
Mgomba wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma
Katibu Mkuu
Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia shughuli za ubanguaji korosho
katika kiwanda cha kubangua korosho wilayani Tunduru.
Katibu wa NEC
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akizungumza na
wafanyakazi wa kiwanda cha kubangua korosho cha Tunduru ambao
walimweleza Katibu wa NEC kuwa wanalipwa kwa wiki na inategemea na idadi
ya kilo ulizobangua.
Katibu Mkuu
Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kuoka kwa meneja wa kiwanda
hicho Ndugu Shinoy jinsi kodi za vyama vya ushirika zinavyokuwa mzigo
kwao na kushauri bora zilipwe kwa mkulima moja kwa moja.
Pichani ni
wafanyakazi wa kiwanda cha kubangua korosho wakiwa kazini katika Kiwanda
cha kubangua korosho cha Tunduru mkoani Ruvuma .
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na mjumbe wa NEC wa wilaya ya
Tunduru Mzee Kalolo,tayari kwa ufunguzi wa ofisi ya CCM kata ya Jakika
jimbo la Tunduru Kaskazini.
Ofisi ya Kata ya Jakika jimbo la Tunduru Kaskazini ambayo imefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Jakika wakati
wa ufunguzi wa ofisi ya kata ya Jakika iliyopo jimbo la Tunduru
Kaskazini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza wananchi wa kata ya Jakika kwenda kuwasha tanuri la kuchomea matofali.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuwasha moto katika matanuri ya
kuchomea matofali katika kata ya Jakika jimbo la Tunduru Kaskazini.
Wananchi wakimpa
mikono Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kama ishara ya
kumkaribisha katika kijiji cha Matemanga wilaya ya Tunduru.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye wakiongoza wananch wa Matemanga kwenda kusaidia shughuli za
ujenzi wa nyumba mbili za madaktari ambazo zinajengwa na Taasisi ya Rais
Mstaafu Ndugu Benjamin Mkapa.
Katibu wa NEC
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimia wakazi
wa kijiji cha Matemanga wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu
Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa salaam za pongezi kwa taasisi ya Rais
Mstaafu Ndugu Benjamin William Mkapa kwa ujenzi wa nyumba mbili za
kuishi madaktari katika kituo cha Afya cha Matemanga wilayani Tunduru.
Katibu Mkuu
Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa mkono wa shukrani kwa fundi Denis Ngaiza
baada ya kutoa ushirikiano wa kutosha katika ujenzi wa nyumba za
Madaktari wa kituo cha afya cha Matemanga.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Milonde
kata ya Matemanga katika kituo cha Kihuma wilaya ya Tunduru mkoani
Ruvuma.
Katibu wa NEC
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro, Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Thabit Mwambungu na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho
wakipitia kwa makini mambo mbali mbali katika nyaraka muhimu za taasisi
ya huduma ya ya kiroho na kibinadamu ya Kihuma iliyopo wilaya ya Tunduru
mkoani Ruvuma
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga kinanda wakati wanakwaya wa kikundi cha Kihuma wakitumbuiza .
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la ofisi ya kata ya
Mlingoti Mashariki wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Sehemu ya umati
uliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM katika viwanja vya Baraza la Eid
wilayani Tunduru ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndgu Abdulrahman Kinana
alihutubia.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia umati wa wakazi wa wilaya ya
Tunduru waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya Baraza la Eid, Nape
aliwaambia wana Tunduru ni jukumu letu kulinda amani ya nchi na kutaka
watu wasikubali kupotoshwa katika mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho akihutubia wakazi wa Tunduru kabla
ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuja
kuhutubia.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa wananchi katika viwanja
vya Baraza la Eid wilayani Tunduru ambapo aliwaeleza wananchi hao kuwa
CCM ni chama cha kutetea haki za wakulima na wafanyakazi na kuwambia
wananchi hao kuwa kila kilichoahidiwa kitatimizwa.
Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Ndugu Thabit Mwambingu akihutubia wananchi wa Tunduru namna
Serikali inavyofungua mkoa wa Ruvuma kwa kuongeza na kujenga barabara na
kuongeza matumizi ya anga.
Mbunge wa
Tunduru Kaskazini Ndugu Ramo Matala akihutubia wakazi wa Tunduru na
kuwaambia taratibu za kuuza zao la korosho kwa pesa taslimu pia namna
anavyosaidia shule na wananchi wakawaida wakiwemo walemavu ambao
alikabidhi baiskeli zao, vifaa vya michezo na kusaidia boda boda kupata
leseni.
Katibu Mkuu Ndugu
Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Ndugu Rajabu Matawaka mara
baada ya kumkabidhi baiskeli ya walemavu iliyotolewa na mbunge ,Mbunge
wa jimbo hilo alitoa vitabu, vifaa vya michezo na madawati 150.
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.